
Home » Posts filed under MICHEZO
Mwanamuziki Diamond Atoboa SIRI ya Wapi Alipoiga Staili ya Kucheza ya Sonkoro Aliyoitumia Kwenye Wimbo Mpya wa Nana soma hapa==>>

Mwanamuziki Diamond Atoboa SIRI ya Wapi Alipoiga Staili ya Kucheza ya Sonkoro Aliyoitumia Kwenye Wimbo Mpya wa Nana.......Ametoboa Siri hiyo Katika Ukurasa wake wa Instagram kwa Kusema Haya Hapa
Diamondplatnumz 'If you Don't know Yet...we Got this #Sankoro Moves from our Legend Brother @fallyipupa01 #NetNaFilm #Nana Watch the Video of that Nana Song by Clicking the Link on my BIO OYa! #Sankoro ABi! KAMA Ronaldo...!!
HII NDIYO LIST YA MASTAA 7 TANZANIA WANAOTEMBELEA GARI ZA KIFAHARI INGIA HAPA==>
Asilimia Kubwa ya mastaa Wa bongo wamekuwa wakionekana wakijivinjari katika mitaa mbali mbali wakiwa katika magari ya kifahari. Lakini ukichunguza utagundua kuwa wengi Wa wasanii hao siyo wamiliki halali Wa magari hayo. Baadhi ya mastaa wanaosukuma ndinga za bei Kali apa bongo ni.
1: DIAMOND PLATNUM
Mwanamuziki anayedaiwa kuongoza kwa kuwa na gari la bei mbaya zaidi nchini ni Diamond Platnums ambaye kwa sasa anamiliki BMW X6 ambalo linauzwa kwa thamani ya dola 62,850 za marekani karibu shillingi million 150 za kibongo.
2: LADY JAYDEE
Anayefuata ni mwanadada lady jaydee anayemiliki magari mawili ya kifahari ikiwemo Nissan Murrano alilonunua kwa thamani ya shilingi mil 60 miaka kadhaa iliyopita na Range rover E lenye thamani ya dola za kimarekani 60,000 sawa ni shilingi mil 100 .
3: AY
Nafasi ya tatu imeshikwa na rapa mkongwe Ambwene yesaya anayemiliki Vogue sports lenye thamani ya sh92 miliion.
4: MASANJA MKANDAMIZAJI
Huyu anamiliki gari aina ya Land cruiser lenye thamani ya shillingi mil. 75
5: MRISHO MPOTO
Namba tano inamilikiwa na mtaalamu Wa mashairi nchini, mrisho mpoto anayemiliki Toyota Prado new model yenye thamani ya shilling mil 65.
6: JACKLINE WOLPER
Kwa upande wake muigizaji jackline wolper anamiliki land cruiser Prado lenye thamani ya shillingi mil 65.
7: WEMA SEPETU
Nafasi ya saba inashikiliwa na mwigizaji wema sepetu anayemiliki BMW 545 yenye thamani ya shilingi million 56, pamoja Na Nissan murrano alilopewa Na aliyekuwa mchumba wake diamond lenye thamani ya shillingi mil 36
Mwana FA: Diamond yuko Sahihi Kutoa Malalamiko yake Kuhusu Tuzo za Kill award soma zaid hapa==>>
Staa wa Hip Hop Bongo,Hamis Mwinjuma amesema kuwa Staa wa Bongo,Diamond ana haki ya kutoa maoni na malalamiko yake kuhusu tuzo za muziki za Kilimanjaro(KTMA) za mwaka huu.
Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena,alisema kilichomtokea Diamond hata yeye kilimtokea wakati alipotoa wimbo wake wa ‘Bado Nipo Nipo Kwanza’ ulifanya vizuri wakati huo lakini jina lake halikuwepo kwenye tuzo hizo.
’Hata mimi nililalamika kama anavyolalamika Diamond lakini niliwaandikia barua Killi wakaniita wakanielewesha kuwa ilikuwa ni makosa ya kibinadamu nikaelewa,’alisema Mwana FA.
Pamoja na hayo amesikitishwa na wasanii Mo Music na Ommy Dimpoz kutokuwepo kwenye tuzo hizo hasa video ya ngoma ya Ndagushima ambayo ilifanya vizuri mwaka jana.
Diamond amelalamikia kutokuwepo kwenye kipengele cha msanii bora wa mwaka,na bendi ya Yamoto kufanya vyema mwaka jana lakini imepata nafasi finyu kwenye tuzo hizo
KAMA ULIKUWA HUJUI HAWA NDIO WASHINDI WETU KWENYE TANZANIA FILM AWARDS ONA PICHA HAPA==>>
Tuzo hizi za filamu, Tanzania Film Awards (TAFA) 2015 zilitolewa usiku wa jana kwenye ukumbu wa wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Da-es-salaam, na hawa ndio washindi katika vipengele vyote 12.
1. Best Actress In Leading Role: Irene Paul
2. Best Comedian: King Majuto
3 .Best Supporting Actress: Grace Mapunda
4. Best Supporting Actor (Male): Tino Hisani Muya
5. Best Screenplay: Irene Sanga
6. Tribute Award (Film Industry Support) : President Jakaya Kikwete
7. Tribute Personality Award: Steven Kanumba
8. Tribute Media : Zamaradi Mketema For Takeone(Clouds TV/Fm)
9. Life Time Achievement Award: Mzee Jangala
10. Best Feature Film : Network
11. Best Director : John Kalaghe
12. Best Actor In Leading Role : Brian Ibrate
PICHA:LAZIMA UIPENDE HILI JUMBA LA KIFAHARI WALILONUNUA JAYZ NA BEYONCE==>
Baada ya kutajwa na jarida la Forbes kuwa miongoni mwa wasanii wa
hiphop wenye mali na matajiri zaidi Jayz na mke wake Beyonce wamehamia
kwenye jumba la kifahari lenye thamani ya pauni milioni 2.6. Jumba hilo
lipo New Orleans Garden, Marekani. Nyumba inavyumba 22.
Jay Z yupo kwenye orodha hio ya Forbes akishikilia namba tatu chini ya Diddy na Dr Dre kwa kuwa na ujaririwa dola milioni 500
MICHEZO HUATHIRI UBIKRA WA WASICHANA??SOMA HAPA KUJUA=>

Mwalimu mkuu
wa shule ya kiislamu mjini Melbourne, Australia amedaiwa kuwazuia wasichana
katika shule hiyo kutoshiriki katika maswala ya michezo kwa hofu kwamba huenda
wakapoteza ubikira.
Wanafunzi wa
kike katika chuo cha Al-Taqwa mjini Truganina pia walizuiwa kucheza soka kwa
kuwa majeruhi huenda yakawafanya kuwa tasa kulingana na fairfax.
Wasimamizi
wa shule hiyo kwa sasa wanachunguza madai hayo yaliowasilishwa dhidi ya Mwalimu
mkuu Omar Hallak ambaye awali alizua hisia kali baada ya kusema kuwa wapiganaji
wa Islamic state walikuwa wakiungwa mkono na mataifa ya magharibi.
Katika barua
iliondikwa na wizara na kuchapishwa na The Age,mwalimu mmoja wa zamani alisema
kuwa:''Anaamini kwamba iwapo wasichana wataruhusiwa kukimbia huenda wakapoteza
ubikra wao.Mwalimu huyo pia ana ushahidi wa kisayansi unaosema kuwa iwapo
wasichana watajijeruhi,kupitia kuvunjika mguu wakati wanapocheza soka huenda
ikawafanya kuwa tasa''..
Mwalimu huyo
amedai kwamba Bwana Hallak aliwazuia wanafunzi wa kike kutoshiriki katika
mashindano ya wilaya ya mbio za marathon mwaka wa 2013 na 2014.
PICHA: RONALDO NDANI YA VAZI LA KANZU!! bofya hapa kuziona picha zake 5===>
Cristiano Ronaldo akiwa kwenye mavazi ya kiislam akipiga picha na mashabiki huko Dubai.
Mchezaji nyota wa mpira wa miguu anaeichezea timu kubwa tajiri duniani Real Madrid alionekana na kupigwa picha na mapaparazi kwenye matembezi yake binafsi Dubai akiwa amevalia mavazi ya Kiislam na yaliompendeza sana.
Cristiano Ronaldo ambaye yeye si Muislam lakini alipendezwa na uvaaji huo kwani alisema aliona watu wengi waishio Dubai ndio vazi lao kuu na kwanini yeye asiwe miongoni mwa waliovaa vazi hilo. Pia hakuwahi kuvaa vazi la dini hiyo alionelea avae kwa ishara ya kuiheshimu dini hiyo na kuona sio kitu kibaya kuwa miongoni kwao kimavazi.

Cristiano Ronaldo akiwa kwenye vazi jingine la kiislamu huko Dubai
Mchezaji huyo alikuwa Dubai wiki iliyopita kwenye mapumziko yake binafsi mbali na shughuli za kimpira. Alienda kutembea huko kabla ya wiki ya sikukuu za christimas. Alionekana ni mwenye kufurahishwa na mandhali ya mji huo pia utamaduni wao wa chakula pia kimavazi ndio mana nae alipendezwa kuvaa kama wao.

Vazi lingine alilovaa mchezaji Cristiano Ronaldo akiwa kwenye matembezi yake binafsi Dubai.
Mchezaji huyo alikaa Dubai kwa siku nne wiki ilopita na baadae aliondoka kurejea Hispania ambapo alijiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya mechi zilizoendelea katika ligi ya ichi hiyo amakochezea
Sakata la Escrow Kaibukia Ndani ya Yanga, Bilioni Mbili Zatafunwa.,,,,soma zaidi hapa==>
Taarifa zilizoufikia mtandao huu wa shaffihdauda.com hivi punde zinadai ya kwamba zaidi ya shilingi bilioni mbili za klabu ya YANGA zimetafunwa na wajanja wasiojulikana mpaka sasa,
Inasemekana ubadhirifu huo umefanyika na baadhi ya wafanyakazi waliomaliza muda wao hivi karibuni,
Baadhi ya majina ya wafanyakazi wa zamani wakiongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo bwana Beno Njovu jana walipelekwa kituo cha polisi cha Central kuhojiwa kutokana na ubadhirifu huo.
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya klabu hiyo kimesema zaidi ya bilioni mbili zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.
Endelea kufuatilia mtandao huu kwa taarifa zaidi
Filed Under:
MICHEZO
on Wednesday, 24 December 2014
Breaking news::David Beckham apata ajali akiwa na mwanae..soma zaidi hapa
Mchezaji mstaafu wa soka wa Uingereza, David Beckham, na mwanae, Brooklyn walihusika kwenye ajali nje ya uwanja wa mafunzo wa Arsenal, ulioko Hertfordshire, Kaskazini mwa mji wa London.
Hata hivyo, hawakupata majeraha bali mshtuko wa kawaida kutokana na ajali hiyo ambayo waligongana na gari nyingine. Habari hizo zilipatikana kutoka kwenye chanzo cha karibu kabisa na familia hiyo. “David na mwanaye Brooklyn hawakupata majeraha kwenye ajali hiyo na ninachojua hata abiria waliohusika kwenye gari nyingine nayo hawakupata majeraha. Lakini wote wanaendelea vizuri,” alisema mtu huyo ambaye hakutaja jina lake litajwe.
Gazeti la Telegraph la Uingereza kwamba mchezaji huyo wa miaka 39 aliyewahi kuwa nahodha wa Uingereza, alikuwa anakwenda uwanjani hapo kumchukua kijana wake mwenye miaka 15 anayechezea timu ya Arsenal ya vijana wenye umri chini ya miaka 16.
Chanzo kingine cha habari kiliongeza kuwa baada ya ajali hiyo kutokea mifuko ya hewa (Airbag) ilifunguka vizuri hivyo kuwasaidia kutopata majeraha yoyote.
BASI UNAAMBIWA HII NDIO SWIMMING POOL YENYE WATU WENGI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA...!!!ITAZAME HAPA
The most crowded public swimming pool is just a mess?? Ladies would you like your boyfriend to take you in such a swimming pool??? The answer to this question is a big NO!
In many African countries we have public swimming pools where people go and just have fun with friends at an affordable fee. Unfortunately in Africa, I have not come across any public swimming pool that strictly upholds hygiene. People pee in the pools and so many disgusting things… Am quite sure that most people who frequently go to such swimming pools end up being infected by skin diseases, Urinary Tract Infections, Fungal/ Yeast infections etc…
It is always good to care of your body. If you must swim and cannot afford to go to a private swimming pool, then why not plan for it, in terms of saving up and then go get a descent treat in a good private swimming pool…You don’t have to risk your body…
Hasheem Thabeet aongea baada ya kuachwa na Pistons....bofya hapa kusoma zaidi
“I came way too far. and i will keep working. I will not stop,” ameandika kupitia Facebook.
Thabeet alikuwa amesaini deal lisilo na guarentee (a non-guaranteed deal) na Detroit Pristons mnamo Sept. 24, baada ya kuachwa na Philadelphia 76ers, ambao walimchukua kutoka Oklahoma City Thunder Aug. 26.
Thabeet—ambaye alishika namba 2 katika 2009 NBA Draft na kuchukuliwa na Memphis Grizzlies—alikuwa mmoja wanne waliotemwa jana Jumatatu na Pistons. Timu hiyo pia imewaacha Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic.
Thabeet alikuwa amesaini deal lisilo na guarentee (a non-guaranteed deal) na Detroit Pristons mnamo Sept. 24, baada ya kuachwa na Philadelphia 76ers, ambao walimchukua kutoka Oklahoma City Thunder Aug. 26.
Thabeet—ambaye alishika namba 2 katika 2009 NBA Draft na kuchukuliwa na Memphis Grizzlies—alikuwa mmoja wanne waliotemwa jana Jumatatu na Pistons. Timu hiyo pia imewaacha Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic.
Filed Under:
MICHEZO
on Sunday, 26 October 2014
Oscar Pistorius na Reeva Steenkamp hawakuwahi kufanya mapenzi – asema Mama Reeva..Kwanini?? soma hapa
Kwenye kitabu hicho, “Reeva: a Mother’s Story”, June Steenkamp aliandika kuwa binti yake alimueleza kuwa pamoja na kwamba walilala pamoja, hawakuwahi kufanya mapenzi sababu Reeva hakutaka kuupeleka uhusiano wao katika kiwango hicho.
Pistorius alihukumiwa miaka mitano jela kwa kumuua Steenkamp bila kukusudia. Alidai alimpiga risasi kupitia mlango wa choo nyumbani kwake Pretoria, February 14, 2013, akidhania ni jambazi.
Gazeti la Sunday Times limeandika kuwa June Steenkamp ameandika kwenye kitabu chake kuwa haamini story hiyo Pistorius. “Alisema kuvuta trigger ilikuwa ajali, Nini? Mara nne ni ajali? Alisema Reeva hakupiga kelele, lakini nina uhakika alipiga kelele. Namjua binti yangu kwakuwa alikuwa na sauti sana,” ameandika kwenye kitabu hicho.
“Hakuna shaka kwenye fikira zetu kuwa kitu kibaya kilitokea, kitu kilichomuudhi Reeva kiasi cha kujificha nyuma ya mlango uliofungwa na simu mbili za mkononi.”
BREAKING NEWZZZZZZZZ! MKATABA WA YANGA, OKWI HAUPO, SIMBA WAWAPIGA BAO WATANI!
Emmanuel Okwi (kushoto) akifanya vitu vyake jana dhidi ya Gor Mahia
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7 mwaka huu) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.
Ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja.
Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.
Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri. Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Hata hivyo mjumbe huyo hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi. Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.
Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda, Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu mfululizo kama takwa la mkataba.
Klabu ya Coastal Union iliwakilishwa na mmoja wa viongozi wake, wakati Banda aliwakilishwa na mwanasheria wake.
Vilevile Kamati imekubaliana na pingamizi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kuhusu wachezaji waliofanyiwa uhamisho kutoka katika mkoa wake bila kulipiwa ada za usajili, hivyo klabu husika zinatakiwa kulipa ada hizo.
Pia Kamati imeagiza klabu zote zilizosajili wachezaji bila kuwafanyia uhamisho, kulipa ada za uhamisho kwa pande husika kabla ya kuanza ligi, vinginevyo leseni zao zitazuiwa hadi watakapolipa.
Mashauri mengine ya pingamizi yatasikilizwa baadaye kwa vile klabu husika hazikupata fursa ya kufika mbele ya kamati.
Kamati inasisitiza kwa wanachama wa TFF kuheshimu mikataba.
Filed Under:
MICHEZO
on Sunday, 7 September 2014