Staa
wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnumz’.STAA wa
muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnumz’ ambaye
aliwatelekeza watoto wawili alioahidi kuwasomesha katika shule ya East
Africa International ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, atashtakiwa
mahakamani endapo wazazi wa vijana hao wataamua kufanya hivyo, Risasi
Mchanganyiko limeelezwa.
Meneja wa msanii huyo, Babu Tale,
awali aliulizwa na gazeti hili juu ya kinachoendelea kuhusiana na vijana
hao waliotimuliwa shule Aprili mwaka huu kwa kutolipiwa ada, lakini
akionekana kupatwa na jazba, alisema wanasikitishwa na jinsi wazazi wa
watoto hao wanavyokiuka makubaliano, hivyo wao hawataki tena kusema
lolote kwa sasa.
“Kama
wao wanadhani kwa kwenda kwenye media (vyombo vya habari) ndiyo watoto
wao watasomeshwa, basi na waende hukohuko watasomeshewa watoto wao,”
alisema Tale aliyeonekana kukasirishwa na mwendelezo wa habari hiyo.
Tale
alitoa kauli hiyo kufuatia mmoja wa wazazi hao wa watoto Hillary na
Hamis, kudai kuwa hakuna maendeleo yoyote ya kulipiwa ada kwa vijana
wao, kwani ingawa waliambiwa mambo yangekuwa sawa baada ya siku chache,
lakini danadana zinaendelea.
Mwanasheria mmoja maarufu nchini
aliyeomba hifadhi ya jina lake, aliliambia gazeti hili kuwa endapo
wazazi wa vijana hao wataamua, sheria zinawaruhusu kumpeleka mahakamani
msanii huyo kwa kukiuka mkataba, hata kama haukuandikwa.
“Makubaliano
ya mdomo ni mkataba unaotambuliwa kisheria, mradi tu wazazi waweze
kuthibitisha, tena kwa hili, inaonyesha siyo tu mkataba, bali inaonyesha
Diamond hakufanya hivyo kwa mapenzi yake kwa watoto, bali baada ya wao
kumfanyia kitu, aliwapeleka shule kuonyesha u-siriazi aliokuwa nao juu
ya ahadi hiyo,” alisema mwanasheria huyo.
Januari mwaka jana, Diamond
aliendesha shindano kwa watoto la kucheza mtindo wa Ngololo na kuahidi
zawadi kwa washindi katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar.
Vijana hao walioshinda, walipewa ofa ya kusomeshwa katika shule hiyo
hadi kumaliza elimu yao ya msingi, lakini tangu wapelekwe hawajawahi
kulipiwa ada.
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI