Ndugu zangu wana UDSM nasikitika kuwapa taarifa kuwa jana usiku wa
saa tano na dakika 20 nilishuhudia mwana UDSM mwenzangu akigongwa na
gari ndogo nyeusi maeneo ya njiapanda ya chuo Ubungo gari iliyombuluza
mita kadhaa kisha kusimama kurudi nyuma na kutokomea kusipojulikana baada
ya makelele tuliyopiga, mbaya zaida gari la pili lililokuwa kasi nalo
likamkanyaga kisha la tatu nalo likamkanyaga ndipo tulipoamua kusimama
katikati ya barabara ilikuzuia maumivu zaidi kwa mtu ambaye MPAKA WAKATI
HUO SIKUJUA NI NANI
Nilikuwa mimi na naibu wangu Joel ntile, tukaamua kukata majani ili
kuzuia magar yaliyokuwa yanakuja kwa kasi kutokana na kutokuwepo kwa
foleni usiku ule katika barabara ya kutoka mwenge kwenda ubungo mataa.
Tukishirikiana na wananchi wengine, tulianza kutafuta gari la kumbeba
huyu mtanzania mwenzetu ambaye mpaka muda huo hatukujua ni nani, lakini
kila tuliyekuwa tukimwomba msaada hakutusaidia na nilipojaribu kupiga
simu polisi haikupokelewa mpaka tukapata akili ya kumkagua
aliyegongwa kujua anandugu na jinsi gani watafika tushirikiane kumpa
msaada, MPAKA MUDA HUO BADO SIKUJUA KUWA NINAYEMSAIDIA NI MWANAFUNZI
MWENZANGU.
Tulipo ipata simu yake tayalri ilikuwa imezimika baada ya kupondwa na
magari matatu, tukatoa line na kuiweka kwenye simu nyingine kila namba
tuliyojaribu haikupokelewa, wakati huo tuliazimia kufunga barabara ili
police wasikie japo kilio chetu na kila tukipiga simu yao iliendelea
kupiga wimbo uleule.
Mpaka tulifanikiwa kupata namba iliyoseviwa shem, tulipopiga alipokea
na nilistushwa na kauli kuwa yupo mabibo na mwenyesimu ni mwanafunzi
mwenzake wa UDSM mwaka wa nne COET, NILIVURUGIKA AKILI
Mpaka muda huo ilikuwa tayari saa nzima imepita bila msaada ndipo
nikapiga simu haraka kwa raisi wa DARUSO mh Ahadi Kitaponda, naye akatuma
gari la wasaidizi wapolisi na dakika chache akaja na ambulance lakini
mpaka muda huo tayali tulikuwa tumechelewa sana na mwana zuoni huyu
alikuwa amesha achana na ulimwengu huu wa shida na mateso,
Polisi walikuja baadae sana kama saa
saba kasoro wakiwa na bunduki na
mabomu mithili wanakwenda kupambana na wahalifu, lakini kuja kwao
hakukusaidia kitu. Ndipo tulianza kuandaa utaratibu wa kwenda
kumpumzisha kwa muda ndugu yetu muhimbili kwa kuanza na dispensari ya
chuo na baadae mida ya saa tisa na nusu tukaingia muhimbili tukiwa na
viongozi wa DARUSO pamoja na jamaa na watu wakaribu wa marehem na mpaka
saa kumi na dakika arobaini tulikuwa tunarudi chuo na hatimaye mabibo."
Alieleza shuhuda huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es
salaam.