MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amewasili
nchini Afrika Kusini leo tayari kwa maisha mapya katika klabu mpya, Free
State Stars ya Bethlehem.
Mchezaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC, Ngassa
ametua Johannesburg leo asubuhi na kuunganisha safari kwa gari la dogo
la Free State kwenda Bethlehem.
Ngassa ametua na mkewe, Radhia Enea Mngazija na watakwenda kukagua nyumba aliyopewa na mwajiri wake, tayari kuanza maisha mapya.
Nimekuja huku kuhamia rasmi sasa, tunakwenda kuangalia nyumba mimi na
bibie (Radhia). Unajua mambo ya nyumba ni ya akina mama. Sasa yeye
akisema ameipenda nyumba, nawaambia safi, tunaingia,”amesema.
Hata hivyo, Ngassa atarejea Dar es Salaam wiki ijayo kwa ajili ya
kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachokwenda kucheza
na Misri mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika katikati ya mwezi.
“Nadhani sitakuwa na muda mrefu, viongozi niliwaambia kabisa natakiwa
kwenye kambi ya timu ya taifa. Kwa hivyo wanajua. Natarajia kurudi wiki
ijayo tu kujiunga na timu ya taifa,”amesema.
Ngassa amejiunga na FS mwanzoni mwa mwezi huu kwa Mkataba wa miaka
minne, kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga SC.
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI