NIjambo la kumshukuru sana Mungu kwa
wapenzi wasomaji wa XXlove kukutana tena, wiki iliyopita tulizungumzia
juu ya hakuna haja ya kuhuzunika kwa kuachwa, bali jipe moyo kwa sababu
utampata akupendaye. Leo napenda tujifunze namna ya kufanya ili kumpata
atakayekufaa kama mwandani wako.
Miongoni mwa fumbo ambalo majibu yake
huwa ni magumu kwa mwanadamu ni suala la kumpata mtu anayefaa katika
uhusiano wa kimapenzi kama mume au mke.Kidunia ni ngumu sana kufumbua
fumbo hilo lakini kwa Mungu ni jambo jepesi na rahisi sana.Kwanza kabisa
kabla ya kutafuta atakayekufaa na kukupenda, wewe binafsi unapaswa
kufanya yafuatayo;
Jiheshimu:
Lazima ujiheshimu kwanza wewe na
wengine watakuheshimu tu bila kujali kipato, elimu, dini au jinsia yako,
lakini kama utakuwa kinyume kila mtu atakuogopa na kukukwepa
kujihusisha na wewe.
Jitambue:
Lazima ujitambue wewe ni nani? Unataka
kuwa na familia ya mama au baba wa aina gani? Kama utajitambua basi
familia yako itakuwa ni ya uzao wa kujitambua.
Jilinde:
Unapaswa ujilinde kitabia na hasa
matendo yako kwa ujumla, ukiangalia vijana wengi sana wanajiingiza
katika uhusiano wa kimapenzi wakiwa bado wadogo.Anayetaka mke au mume
huwa anaangalia namna unavyojilinda ili hata kama akikufanya mke au mume
hatakuwa na wasiwasi juu ya kukulinda kwani anajua unaweza kujilinda.
Acha umapepe:
Vijana wengi wanaonekana kuwa ni mapepe
na wasiotulia ndiyo maana hata suala la ndoa ni gumu kwa kizazi cha
sasa. Hii inasababishwa na vijana kurukaruka sana na kusahau kuwa kuruka
huko kuna shida siku za usoni kama si magonjwa ya zinaa, utasa, ugumba
basi kifo au kukosa mke au mume.
Kwa mtu anayetaka kuoa au kuolewa ni
lazima huanza kwa kuichunguza familia ya muoaji na muolewaji kwanza
kisha mlengwa na kama ikibainika hata wazazi wake walikuwa ni waluwalu
basi hakuna muoaji au muolewaji.
Sidhani kama kuna mzazi anapenda
mwanaye akateseke katika ndoa yake kama pengine alivyowahi kuteseka au
kuona familia nyingine ikiwa katika hali hiyo.
Unaukumbuka wimbo wa “Manunga embe’’
ulioimbwa na Kundi la Zig Zaga Crew, kuna sehemu inasema “Wanawake
wazuri wazuri wazuri wameolewa, yamebaki manunga embe yanahangaika’’
kimtazamo wimbo ule ulikuwa unazungumzia tabia nzuri ya mwanamke ndiyo
inaweza kumfanya akapata mume, hata mwanaume vilevile.
Tukutane wiki ijayo katika sehemu ya pili ya mada hii.
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI