Vanessa Mdee amesema anawashangaa wasanii wa Tanzania na Afrika kwa
ujumla wanaolalamika kuwaona wasanii wao wakipewa tuzo kabla ya show ya
BET Awards.
Vanessa Mdee ambaye ni mmoja wa majaji wa tuzo hizo, amekiambia kipindi
cha XXL cha Clouds FM kuwa BET wanashindwa kuonesha jinsi wasanii wa
Afrika wanavyokabidhiwa tuzo kutokana na sababu za kibiashara na
wadhamini.
“Unajua watu wanasahau kama zile tuzo sio za waafrika, it’s for African
American,” amesema Vanessa. “Halafu ujue wale sio kama Kili, labda Kili
wanapewa three hours halafu wanaongezewa kama nusu saa au dakika 15
wakiwa wanaonyesha kwenye TV. Wale two hours it’s two hours, ikizidi
inakatwa, so lazima wavute watu ambao wataongeza viewership nyingi,”
ameongeza.
“Marekani network zinalipwa kwa viewership, ndio maana unaambiwa rate ya
show fulani ni kubwa, wana-monitor watu wangapi wanatazama, wanaget
more money kupitia watu wanaowatazama. Kwahiyo wanajaribu kuvuta
Wamarekani zaidi. Sasa kitendo cha msanii wa Afrika, Marekani anawajua
waafrika? Hawajui, so tukilalamika tunakosea, kwa sababu hiyo tuzo sio
za kwetu. Ndio tunataka na sisi tuonekane but it’s not our show na
huwaingizii hela na mpaka tufikie hapo tushukuru hata wametupa hicho
kipengele.”
“Ukiaangalia hata Chris Brown tuzo yake haikugawiwa pale kwenye stage,
ni kwamba alishinda viewerS choice award ndIO akaenda akapokea viewers
na ile nyingine. Za Beyonce uliona hata mtu mmoja ameenda kupokea pale
kwenye stage? No, hata za kwao ziligawiwa red carpet. Kuna tuzo nyingi
ambazo zinagawiwa mwanzoni,” alisisitiza Vanessa.