Mimi ni kijana ninaeishi na kufanya kazi Dodoma, mwezi desemba nilienda
kumtembelea binamu yangu alieolewa Dar es salaam, anaishi maeneo ya
ukonga.
Kuna matukio yanayotokea na kunishangaza,sasa chumba anacholala binamu
yangu na mme wake vinapakana na choo na bafu kama mara tatu hivi wakat
naenda bafuni kuoga nilimkuta binamu yangu kaacha mlango wazi huku yuko
uchi nikageuka haraka nikarudi nilikotoka.
Mara ya pili binamu yangu alikua ametoka chooni, sasa mimi nilikua
naenda kuoga nikamwona bwana akiwa uchi, mara ya tatu tena alikua uchi
chumbani huku ameacha mlango wazi cha kushangaza alipogundua
hakuhangaika kujisitiri aliendelea na mambo yake,nilipogeuka kumkwepa
ndio nikasikia samahani huku yupo very relaxed.
Sijui nifanye nini wadau,msaada tafadhali