BARAKA!
Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu Bongo,
Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha
Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake
huo.
Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote
ule ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti
maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni
haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba
yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo
chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni
halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,” alisema Nape.
Hata hivyo,
alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho
hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye
shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka 2010.
Wasanii
wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya Wema
ni Ndumbagwe Misayo ëTheaí (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara Juma
(Viti Maalum Morogoro Vijijini)
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI