OMARY Faraji Nyembo,
anayefahamika zaidi kimuziki kama Ommy Dimpoz ni msanii mwenye jina
kubwa katika fani, ingawa ni miongoni mwa vijana waliochipukia na kupata
umaarufu katika miaka ya hivi karibuni.
Amefanya kazi nyingi
nzuri na zilizopata kupigwa sana katika vituo vingi vya redio na
televisheni, baadhi yake vikiwa ni pamoja na Baadae, Me and You,
Ndagushima na Wanjera, kitu kinachomfanya kuwa miongoni mwa wasanii
wanaofanya vizuri katika soko la Bongo Fleva kwa sasa.
Ingawa hatambi sana,
lakini uwezo na kazi zake kwa sasa unamfanya kuwa mmoja wa wasanii ambao
kukosekana kwake katika shughuli yoyote kubwa ya burudani ni kero kwa
mashabiki. Anategemewa kuwepo miongoni mwa vijana kumi bora wa muziki wa
kizazi kipya.
Kwa upande wake, Martin
Kadinda ni miongoni mwa wabunifu vijana wa mavazi hapa nchini, ingawa
fani hii haimpi jina sana kama ile ya kuwa meneja wa muigizaji Wema
Sepetu. Lakini kiukweli, Martin yupo sana kwenye ubunifu na mitindo.
Nimemfahamu kitambo
kidogo, akishiriki kupanda jukwaani kusindikiza nguo zilizobuniwa naye
au ‘dada zake’ Khadija Mwanamboka na Asia Idarous au wabunifu wenzake
akina Ally Rhemtulah. .
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI