Wakati vyombo vya usalama duniani vikitumia kila njia kuhakikisha kuwa
biashara ya dawa za kulevya inakomeshwa, wasafirishaji nao wamekuwa
wakibuni mbinu mpya kila siku.
Hata hivyo, mbinu za wafanyabiashara hao zimekuwa zikifichuliwa kwa
kutumia vifaa maalum, kama kamera na mbwa wanaokuwapo kwenye viwanja vya
ndege na mipakani. Vifaa hivyo huweza kuona au kunusa vitu
vilivyofichwa ndani ya mabegi, makopo hata tumboni.
Gazeti la The Telegraph la Uingereza limekusanya baadhi ya picha
zinazoonyesha mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wahalifu kusafirisha
‘unga’. Baadhi ya picha zinaonyesha dawa za kulevya zikiwa ndani ya
maparachichi, mananasi, tumboni mwa watoto wa mbwa waliokuwa
wakisafirishwa.
Pia, baadhi ya wasafirishaji hao waliibuka na mbinu mpya za kujifunga
tumbo la ujauzito wa bandia lililosheheni cocaine, huku wengine
wakijifunga mwili mzima mifuko ya dawa hizo.
Ritchie Tabatha Leah, raia wa Canada, alinaswa kwenye Uwanja wa ndege wa
Bogota Septemba mwaka 2013 akiwa amejifunga tumbo la bandia ili
aonekane mjamzito, lakini alipopekuliwa muda mfupa kabla hajaingia
kwenye ndege alikutwa na kilo2 za dawa aina ya cocaine.
Genge la wauza dawa za kulevya waliwafanyia upasuaji watoto wa mbwa
kisha kuwabebesha dawa za kulevya aina ya heroine. Hata hivyo, mpango
huo ulivurugika baada ya polisi kuubaini kupitia kamera maalumu.
Picha za X-ray zilionyesha mifuko iliyowekwa dawa za kulevya tumboni mwa
mmoja wa abiria aliyenaswa katika mmoja ya mipaka ya Uingereza wakati
akijaribu kuingiza ‘mzigo’ huo.
Askari wa Colombia waliokamata nyambizi kwenye mji wa Timbiqui baada ya
kuihisi imebeba dawa hizo, walibaini ilikuwa imebeba tani 8 mwaka 2011.
‘Unga’ huo ulikuwa ukipelekwa Mexico.
Mtu mwingine alikamatwa na maafisa wa forodha kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kabul nchini Afghanstan akiwa amejiviringisha mwilini dawa za kulevya
aina ya heroine zenye uzito wa kilo 7 Juni 2007.
Polisi nchini Hispania walifanikiwa kukamata kilo 200 za cocaine zikiwa
zimefichwa ndani ya nanasi ambalo lilikuwa limesafirishwa kutoka kutoka
Marekani. Nanasi hilo lilipatikana ndani ya moja ya makontena 10
yaliyokuwa yamewasili kutoka bandari ya Algeciras.
Raia wa Chile mwenye umri wa miaka 66 aliyekuwa amevaa bandeji ngumu
inayotumika kufunga mtu aliyevunjika, alikamatwa kwemye Uwanja Ndege wa
Barcelona mwaka 2009 baada ya kubainika kuwa hakuwa mgonjwa bali alikuwa
amebebwa dawa za kulevya.
Parachichi lililosheheni dawa za kulevya aina ya cocaine likiwa limepasuliwa baada ya polisi kulitilia shaka.
Wakati mwingine huonekana kama mayai, lakini ukweli ni kwamba hayana
ladha ya mayai. Mtu aliyebeba mzigo huo alikamatwa na maofisa uhamiaji
wa Marekani. Mtu huyo, Esteban Galtes alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Los Angeles akiwa na cocaine.
Mwanasesere aliyekuwa ametumwa kupeleka kitu kama zawadi nchini
Australia kutoka Sydney mwaka 2007, alinaswa na maofisa wa kupambana na
dawa za kulevya baada ya kubainika dawa za kulevya zilikuwa zimefichwa
ndani yake.
Mfuko wa James Bettridge uliokuwa na cocaine ulikamatwa na maofisa wa
polisi Agosti mwaka jana nchini Uholanzi muda mfupi baada ya kuwasili
kutoka Ufaransa.
Tani 15 za dawa za kulevya aina ya bangi zilikamatwa baada ya polisi kuzing’amua ndani ya kontena.
Dawa nyingine zilikamatwa zikiwa ndani ya boksi la maji ya kunywa
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI