WAKATI
binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu
salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa
kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu
katika mfumo wa jua. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya
internet,
sayari
iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani
kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa
mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea
dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani
na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa
zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi
kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi
kuongezeka sehemu mbalimbali. Mbali na dunia kutikisika na matetemeko,
milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo
mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe
dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani. DUNIA
ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati
volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza,
dunia itafunikwa na giza nene na matope kwa wakati wote wa usiku na
mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na
Zephaniah 1:14-17. NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru
inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha
madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko
usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini
kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo
sasa). WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi
ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa
kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa
masuala ya nyota. MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa
mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy
Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto
kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na
kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya
kizazi cha binadamu. Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na
ukubwa wa mara nne ya dunia. BAADA YA NDOTO
Baada
ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark
Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001
alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa
dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12,
wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi)
6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12.
Nibiru. IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata
hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New
York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza
lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa
dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir,
hivyo kuiachia dunia anayoishikilia. Wamesema baada ya kuiachia dunia
itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi
ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye
Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya
mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba. Makanisa mengi nchini Tanzania
yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni
Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama
Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe. FREEMASON WABARIKI
Jamii
ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia
inatarajie tukio kubwa la pamoja. Mitandao ya jamii hiyo inataja kama
hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani
kushindania watu huku waendao upotevuni wakiwa wengi. MFUMO WA DUNIA
TANGU KUUMBWA
Kwa
mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu
kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000
(inaweza isitimie au ikapita kidogo). Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva
mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo
wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi
saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika
tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI