NI laana! Baadhi ya mastaa wamenaswa laivu wakifanya vitendo vilivyotafsiriwa kuwa vya kifuska, Ijumaa Wikienda lina mkanda kamili.
Baadhi ya mastaa wakionyeshana ufundi wa kucheza.
Tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya Victoria, Dar wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto wa mjini, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’.
...Ilikuwa ni full kukata mauno ndani ya Letasi Lounge.
Likishuhudia tukio hilo, Ijumaa Wikienda ambalo lilijipenyeza ndani ya nyumba, lilifuatilia kila aina ya tukio huku likifikisha ripoti kwa mkuu wake ambaye alikuwa ofisini akipokea matukio ya Live Dijitali.
...Burudani baada ya kukolea, hali ilikuwa hivi.
Ndani ya ukumbi huo lilishuhudia laana za aina yake ambazo zilikuwa zikiongozwa na mwenye shughuli ambaye alikuwa akikata mauno ya ajabu kwa staili ya ‘baba na mama’ chumbani.
Husna Maulid akionyesha ufundi.
“Duh! Yaani utafikiri watu hawajui kuwa hii ni Kwaresma, ni full laana hebu angalia Husna Maulid, Sajent (Husna Idd) na Davina (Halima Yahya) wakiongozwa na Muna wanavyojichetua hadi ‘makufuli’ yanaonekana,” alisema mwanadada mmoja.
Katika hatua nyingine, mwanaume tata anayejulikana kwa jina la Agrey alivua nguo na kubaki na ‘kufuli’ kisha alipanda juu ya kiti na kuanza kuonesha staili mbalimbali za ukataji wa mauno.
“Tobaa… jamani mwangalieni Agrey, kavua nguo anamwaga radhi…hahahaaa,” alisikika msanii mmoja wa Kundi la Vituko Show.
...Sajent na Husna wakizidi kujiachia.
Kingine kilichojiri ni pale shindano lisilokuwa rasmi la kuzungusha nyonga lilipoibuka kati ya watoto wa Ilala linaloongozwa na Baby Tunu na Baby Tau ambao walishindana na watoto wa Kinondoni, Sajenti na wenzake, hali iliyosababisha watu kushindwa kuvumilia na kuinuka vitini.
Ili kunusuru hali, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Chumi Suleiman ‘Bi Hindu’ alilazimika kuzima muziki kuepusha laana iliyokuwa inazidi kuvuka mipaka.
“Jamani hata mimi nina watoto wa kiume na kike, sasa hii hali siwezi kuivumilia, nazima muziki na shughuli ndiyo imemalizika maana wote humu ndani tutaonekana siyo,” alisema Bi Hindu ambapo baada ya kusema tu, aliambulia mvua ya matusi.