Featured

Jokate Mwegelo asaini mkataba wa thamani ya Sh8.5 bilioni na kampuni ya Kichina...soma zaidi hapa==>>

Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006,  mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.Makubaliano hayo yalisainiwa jana kwenye hotel ya  Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun.
 
Akizungumza katika hafla hiyo,  Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.
 
Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.
 
 “Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa, lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.
 
Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na  mawigi,  weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals) ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania. 

“Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema. 
 
Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao na Tanzania.
 
 “Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.

 Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini
Jokate na Guoxun wakibadilishana mikataba baada ya kusaini
Jokate akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo

Meya wa Manispaa ya Ilala akiteta jambo na Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mariam Kisangi katika hafla hiyo.
Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip KUJUA SEHEMU 12 ZINAZOMPA RAHA MWNAMKE WAKATI WA TENDO BONYZA HAP CHNI
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA ZA MAPENZI Published.. Blogger Templates
Back To Top