Watu wakiwa kwenye fukwe ya bahari ya Hindi Coco Beach. Msimuu huu wa sikukuu za Krismasi na mwaka Mpya watu wengi hupendelea kwenda kupumzika katika fukwe mbalimbali ikiwa ni sehemu moja wapo ya kusheherekea sikukuu hizo bila kujali kuwa idadi kubwa ya watu huhudhulia katika fukwe hiyo kwa lengo la kuburudika.
Kesho ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo (Kristmas) ambapo watu wengi hukamilisha siku hiyo kwa kula vyakula mbalimbali ambavyo huashiria kuwepo kwa furaha kwa siku hiyo lakini imebainika kuwa kati ya fukwe zinazo ongoza kwa kuhudhuliwa na watu wengi zaidi jijini Dares salaam ni fukwe ya coco (Coco Beach).
Kama huamini hilo basi ni vema siku ya kesho ukachagua fukwe ya coco ( Coco Beach) kuwa sehemu ya kufurahia sikukuu ya Christmas ambapo utathibitisha kuwa fukwe hiyo ni tishio jijini Dar es salaam kwa wapenda burudan


