Mwalimu mkuu
wa shule ya kiislamu mjini Melbourne, Australia amedaiwa kuwazuia wasichana
katika shule hiyo kutoshiriki katika maswala ya michezo kwa hofu kwamba huenda
wakapoteza ubikira.
Wanafunzi wa
kike katika chuo cha Al-Taqwa mjini Truganina pia walizuiwa kucheza soka kwa
kuwa majeruhi huenda yakawafanya kuwa tasa kulingana na fairfax.
Wasimamizi
wa shule hiyo kwa sasa wanachunguza madai hayo yaliowasilishwa dhidi ya Mwalimu
mkuu Omar Hallak ambaye awali alizua hisia kali baada ya kusema kuwa wapiganaji
wa Islamic state walikuwa wakiungwa mkono na mataifa ya magharibi.
Katika barua
iliondikwa na wizara na kuchapishwa na The Age,mwalimu mmoja wa zamani alisema
kuwa:''Anaamini kwamba iwapo wasichana wataruhusiwa kukimbia huenda wakapoteza
ubikra wao.Mwalimu huyo pia ana ushahidi wa kisayansi unaosema kuwa iwapo
wasichana watajijeruhi,kupitia kuvunjika mguu wakati wanapocheza soka huenda
ikawafanya kuwa tasa''..
Mwalimu huyo
amedai kwamba Bwana Hallak aliwazuia wanafunzi wa kike kutoshiriki katika
mashindano ya wilaya ya mbio za marathon mwaka wa 2013 na 2014.