Kukosekana kwa Waziri na pia mwanasheria Mkuu kujiondoa wote wakiwa wanaiwakilisha Zanzibar ,wajumbe walio wengi wameichukulia hali hiyo kama kujitoa kwa Zanzibar katika kutunga Katiba mpya kwani itakosa nguzo muhimu zinazohitajika kutoka pande mbili za nchi washirika wa Muungano.
Sababu zinadaiwa kujitoa kwa viongozi hao wakuu ni kutokana na mwenendo mzima wa kutunga Katiba ambao umekumbatiwa na Chama tawala kwa maslahi yao binafsi na kuondoa ile hali ya kuifanya Katiba hiyo iwe inatokana na maoni ya Wananchi kama yalivyowasilishwa kwenye rasimu ya Jaji warioba na tume yake ambayo imesainiwa na raisi wa Jamhuri wa Muungano. CCM hawakujali saini ya Raisi wala ghali wameutupilia mbali na kuchomeka waliyokuja nayo kwenye viroba.
wakuu hao kwa kuthamini taaluma yao ya uwana sheria hawakuwa tayari kushiriki kusaidia hila za CCM kugeuza na kupindisha maoni ya wananchi taaluma yao haiwaruhusu na hivyo wamejiengua kulinda heshima yao na vilevile kutokubali kuiwakilisha Zanzibar katika uchakachuaji wa Rasimu ya Jaji Warioba na tume yake ambayo imesainiwa na Raisi.
Inasemekana pia wakuu hao kabla ya kujiengua walimueleza Raisi wa Nchi yao kile kinachoendelezwa na kufanywa na CCM ndani ya bunge hilo la katiba na kuwa wao hawapo tayari kuendelea kukaa na kuandika jambo ambalo lilimpelekea Raisi wa nchi yao Nheshimiwa Sheini wafanye vile wanavyoona wao ndivyo ili kulinda maslahi ya Zanzibar na watu wake. Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Kwa Haraka: BONYZA HAP CHNI