Katika kijiji cha Kiegei kila tarehe 25 ya mwisho wa mwezi, baada ya mnada wa bidhaa mbalimbali za kilimo kama chakula na vifaa vya nyumbani kama vyombo.
Watu wengine, wekiwemo watoto wa shule za msingi huuziana mabusu na wafanyabiashara wa mnada huo, kusababisha kukatisha masomo kwa baadhi ya wanafunzi kwa kushika ujauzito na wengine kupata magonjwa ya kuambukiza kama gono, kaswende na Ukimwi.
Baada ya kuuza bishaa zao mbalimbali katika mnada huo, unaohusisha wafanyabiashara kutoka katika wilaya za jirani kama Liwale, Tunduru na Masasi, wafanyabiasha wa Kiegei huingia katika vibanda vya sinema, mathalani kuangalia filamu mbalimbali, lakini humo ndani ya vibanda filamu hutumia pesa zao kununua ngono kutoka kwa watoto.
Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 inalenga kuhakikisha kwamba watoto wote wanastawi na kuwa na maisha bora, kutokana na kupatikana kwa haki zao za msingi ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa katika mambo yanayowahusu bila ua ubaguzi wa hali yoyote.
Kwa mujibu wa sera hiyo, mtoto ni yule mwenye umri wa chini ya miaka 18. Mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 anastahili kulindwa na familia yake pamoja na wanajamii wanaomzunguka ili kumuangalia ukuaji wake uwe wenye usalama zaidi.
Madhara ambayo anaweza kuyapata mtoto kama hajapata uwangalizi kutoka katika familia yake na jamii inayomzunguka ni, kuathirika kiafya, kiakili, kimwili, kihisia na kijinsia.
Pia pale ambapo maendeleo ya mtoto yanavurungwa, ni pale uhai wa mtoto uko hatarini pamoja na utu wa mtoto unapokosekana.
Sheria ya kimataifa ya mwaka 2009 ya kutetea watoto kutoka umoja wa mataifa inaeleza kuwa, mtoto wa chini umri wa miaka 18 anatambulika kama mtoto kidunia na anastahili kulindwa na familia yake na kupewa mahitaji muhimu kama chakula bora, maradhi, nguo na elimu bora, mtoto huyu atakiwa kuanza kujitegemea yeye mwenyewe au kuachiwa huru kufanya ngono zembe na ajira majumbani na mashambani ili alishe familia hairuhusiwi kimataifa.
Lakini, ukitembelea vibanda vya sinema vya kijiji cha Kiegei kuanzia saa 12.00 jioni, utawakuta watoto wa kike, wenye umri kuanzia 10 hadi 14, katika shuguli mbali mbali za kutafuta hela kwa kuuza ngono.
Siku ya tarehe 25 Januari, 2013, ambayo ilikuwa ni siku ya ijumaa, zikioneshwa sinema za kivita mbili, wasichana wapatao 10 walionekana ndani ya kibanda cha sinema kilichopo katika kijiji cha Kiegei, wakipakwatwa na kushikwa-shikwa na wanaume wenye umri mkubwa.
Saa 6:00 usiku, kila mtoto alitoka na mwanaume na kuelekea sehemu mbalimbali kama vyoo vya shule ya msingi Kiegei, uwanja wa mpira na wengine kwenye meza za mchezo wa pool, iliyopo katika Soko dogo la kijiji cha Kiegei na wengine pembezoni mwa jengo la Kanisa.
Mtoto huyo na mwanaume mtu mzima wakiwa katika meza ya mchezo wa pool, wakaanza kufanya ngono mbele ya macho yangu, bila hata ya kuona aibu yoyote, tena bila hata huruma kama anayefanya naye ngono ni mtoto wa shule ya msingi.
“Kama unaona mwenzio anafaidi na tendo hili la ngono basi njoo weye mtu mzima ufanye;naona umeshangaa kwa kutoa macho utazani hujui nini kinachofanyika hapa,” alisema jibaba hilo huku akiendelea kufanya ngono na kitoto hicho.
Saa 12:00 asubuhi kesho yake, hakukukuwa na mabaki ya kondom katika maeneo haya yote.
Kwa mujibu wa wanafunzi wa shule ya msingi Kiegei, wanalipwa kiasi cha sh.500 hadi sh.2000 kufanya ngono na watu wazima.
“Nimeanza ngono nikiwa na umri wa miaka 12, kabla hata sijabalehe nafanya ngono na wanaume wakubwa ambao ni wachimbaji wa madini Mbwemkuru na wafanyabiasha ya mnada wanaofika kila tarehe 25 ya mwisho wa mwezi, kwa ujila wa Tshs. 500 hadi Tshs. 2000 kwa siku,” alisema Anna Peter (13) sio jina lake
Wakati huo huo, mwalimu mkuu wa shule ya Kiegei, Fred Mchekenje, alisema kuwa wanafunzi wa shule yake bado hawajaanza kufanya ngono kwani bado wadogo sana na kudai kwamba mambo hayo wanafanya watoto wa mitaani.
“Bado wadogo sana; hawajaanza kufanya mambo hayo ya kiutu uzima. Wanapenda kusoma na muda mwingi wako nyumbani wanajisomea wakitoka shuleni,” alisema Mchekenje.
Mchekenje alisema kuwa, mwaka 2012 wanafunzi wapatao 29, walifanya mtihani wa kumaliza darasa la saba, kati ya hao wanafunzi 29 walifaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Kiegei, kati ya hao wasichana 11 na wavulana 18.
Mwaka 2011 wanafunzi walifaulu walikuwa asilimia 70 na wakapata fulsa ya kujiunga na masoma ya sekondari na vyuo vya ufundi stadi veta.
Asilimia 30 ndio waliobaki mtaani ambao hawakufaulu na kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari katika shule mbalimbali za sekondari Nachingwea.
Aidha alisema kuwa matokeo ya darasa la nne yalikuwa mabaya sana kwa mwaka 2012; waliofanya mtihani walikuwa 95 na waliofaulu ni watoto nane tu. Kati ya hao, wavulana walikuwa sita na wasicha ni wawili. Kwa mujibu wake, sababu kubwa ya kufeli ni kutokuwepo kwa vitabu, chaki na upungufu wa walimu; badala ya 15, kwa sasa wapo watatu.
Mchekenje alisema kuwa mahudhurio ya watoto wa kike shuleni ni mazuri na hakuna mimba iliyopatikana kwa miaka saba sasa; mara ya mwisho kumpata mtoto mwenye ujauzito ni mwaka 2006. Anadhani sababu kubwa ya kupungua kwa mimba shuleni ni kuwepo kwa somo la elimu lika lililoanza kufundishwa mwaka 2007.
Kwa mujibu wa Juma Ramadhani, ambaye ni mkazi wa kijiji hicho na mzazi wa watoto watatu wanasoma katika shule ya msingi Kiegei, mwaka 2012, wanafunzi wawili walipata mimba wakiwa darasa la sita na kukatisha masomo yao.
Kama Anna, Salima Musa (sio jina lake) ni mwanafunzi wa shule ya msingi. Mtoto huyu, amabye ana miaka 11 na yuko darasa la tano katika shule ya msingi Ukombozi anasema, “Nimezoeya kufanya ngono na watu wazima. Sitaki watoto wa shule wenzangu kwa sababu wananuka mkojo; nataka wanaume wenye misuri iliyokomaa kwani ndio nasikia raha zaidi.”
Aziza Ally (siyo jina lake) aliacha shule mwaka huu, akiwa darasa la sita. Hana ndoto tena za kwenda shule maana ngono anayofanya ndio inampa uwezo wakuilisha familia yake kwa sasa.
“Sijawahi kutumia kondom toka nimeanza kufanya ngono nikiwa darasa la nne. Kwa sasa nimeamua kuacha shule kwa sababu walimu wameniamba nirudie darasa la tano badala ya kuwa darasa la sita.
Nimeona bora nifanye ngono ili nijikimu kimaisha kwa kujinunulia nguo, viatu na mafuta mazuri pamona na kutoa nyumbani pesa ya chakula. Hapa unaponiona nimetoka kumaliza dozi ya ugonjwa wa gono wiki moja iliyoisha na sasa niko mawindoni natafuta pesa.”
Baba yake Aziza aliki kufahamu kwamba mtoto wake anajihusisha na ngono zembe.
“Nimemkanya asifanye ngono lakini hasikii. Nimeamua kumuacha tuu ila kwa sasa sina huduma yoyote ninayopa mtoto huyo; anajinunulia mwenyewe nguo za kuvaa, mafuta ya kupaka na chakula,”alisema Baba yake Aziza.
Kwa mujibu wa Dk. Kahabi Isangura, mtaalamu wa magonjwa ya kijamii, kuna madhara makubwa sana kwa mtoto kuanza kufanya ngono katika umri mdogo. Anaweza kupata mimba na kukatisha ndoto zake za kusoma, anaonekana muhuni pamoja na kukabiliwa na majukumu makubwa akiwa na umri mdogo.
Dk. Isangura alisema kuwa madhala ya kiafya ni kama kupata magonjwa ya kuambukiza yakiwemo ukimwi, gono, kaswende na kisonono. Pia, anaweza kupata kansa ya kizazi kwa kuanza ngono mapema kwa sababu seli za kingo za uke zinakuwa hazijakomaa vema, hivyo nirahisi kupata majereha na kuweka ufa ambao unasababisha kupata kansa ya kizazi akiwa mtu mzima.
Ngono ya utotoni husababisha vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kwa sababu mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 14 nyonga yake ya uzazi inakuwa bado haijakomaa kusukuma mtoto wakati wa kujifungua, hivyo basi kunauwezekano mkubwa wa mtoto huyu kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mganga wa Zahanati ya Kiegei Olafu Chinguile, mwaka 2011 wagonjwa 48 walifika wakiwa wanaumwa magonjwa ya Kaswende na Gono; kati ya hao watoto walikuwa 5.
Mwaka 2012 wagonjwa waliofika katika zahanati yake wakiwa wanaumwa magonjwa ya Gono na Kaswende walikuwa 38; kati ya hao, nane walikuwa watoto kati ya miaka 10 na 14.
Habiba Juma alimaliza darasa la saba katika shule ya msingi kiegei mwaka 1994 na kusema kuwa, kipindi alichokuwa anasoma yeye hakukuwa na mambo ya ngono kwa wanafunzi na watu wazima, lakini ilipofika mwaka 1995 ndio mambo ya ngono kwa wanafunzi yalipoanzia baada ya kuanza kwa machimbo ya madini.
Makwasa Bulenga ni Afisa elimu wa shule ya msingi wilaya ya Nachingwea alisema kuwa,tatizo kubwa la wanafunzi kufanya ngono ni kuwepo kwa vibanda vya kuonesha sinema mbalimbali muda wa usiku.
“Vibanda vya sinema kwa vijijini ndio tatizo kubwa kwa watoto wa shule ya msingi kujifunza mambo machafu, huku sinema hizo wakiangalia na watu wazima tena wanaume hasa wachimbaji wa kutoka sehemu mbalimbali za uchimbaji,”alisema Bulenga
Bulenga alisema kuwa ofisi yake imewaita mara kadhaa viongozi wa vitongoji na vijiji kuwaeleza umuhimu wa vibanda vya sinema kufungwa mapema, lakini juhudi hizo zimegonga mwamba kwa sababu vibanda hivyo vinaanza kuonesha sinema kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku na wateja wao wakubwa ni watoto wa shule za msingi.
Vibanda vya sinema vinatakiwa kuanza kuonesha sinema saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni.
“Sio tuu kiegei watoto kufanya ngono; na vijiji vingine pia hali ni hiyo hiyo kama uliyoishudia kiegei, bado tupo katika hali mbaya sana kwa watoto kuanza ngono mapema kwa wilaya ya Nachingwea,” alisema Bulenga.
Kwa mujibu wa Bulenga, katika wilaya ya Nachingwea kuna kata 32; kati ya hizo, kata sita pekee ziko mjini. Nyingine zote ziko vijijini na sehemu kubwa yake ndio kuna wanafunzi wengi ambao wanafanya ngono baada ya kumaliza kuangalia sinema za ngono katika maeneo hayo.
Mjini kuna wanafunzi wapatao 4,789; wavulana ni 2,365 na wasichana 2,424. Vijijini kuna wanafunzi 27,047; kati yao, wavulana wako 13,319 na wasichana ni 13,728. Walimu waliopata mafunzo kuhusu somo la elimu lika kwa wilaya ya Nachingwea wako 23; wanaume 14 na wanawake9.
Inapaswa kuwa na walimu ambao wamepatiwa elimu lika 300, ili kiweza kukidhi idadi ya wanafunzi wa shule za mjini na vijijini katika wilaya ya Nachingwea kwa sasa.
Walimu ambao hawakupata mafunzo lakini wanafundisha somo hilo la elimu lika wako 200; wanaume 116 na wanawake 84. Hii inachangia uwajibikaji mdogo kwa walimu ambao hawajapatiwa mafunzo ya somo hilo jinsi ya kumfundisha mwanafunzi akajiepusha na ngono.
Kwa upande wake, Jane Mrema mshauri wa masuala ya jinsia na kutetea haki za watoto na vijana kutoka Plan International alisema kuwa, tatizo la shule ya msingi Kiegei kwa watoto kuanza ngono halifahamu.
Mrema alisema kuwa watoto wanalengwa na shirika la Plan International ni kuanzaia mwezi mmoja mpaka miaka 18, hasa kwa watoto wa kike pamoja na walemavu. Kwa sasa wanafanya kazi katika mikoa mitano nayo ni Mwanza, Geita, Morogoro, Pwani na Dar es salaam lakini pia wanafanya katika wilaya sita ambazo ni Kibaha, Kisarawe, Kilombero, Sengerema, Ilemela, Geita na Ilala.
“Tunamuelisha mtoto wa kike kutambua haki yake ya kupata elimu bora na afya bora, pia mtoto kufahamu unyanyasaji wa kijinsia majumbani na njiani akienda shuleni, pamoja na kuangalia mazingira ambayo yapo hatarishi kwa kupata unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto wa kike,” alisema Mrema.
Aidha Plan International wamejenga mabweni katika wilaya mbalimbali kama Ilala katika shule ya sekondari sakara, kibaha shule ya sekondari ya ruvu, mwanza na geita kila bweni linauwezo kuchukua watoto 100, pia wamejanga choo na mabomba ya maji safi.
Kwa sasa kuna kampeni nyingine ijulikanayo kama kwa sababu mimi ni msichana ambayo lizinduliwa mwishoni mwezi wa Octoba mwaka jana, lengo kubwa la kampeni hii ni, kuhamasisha jamii kutetea haki za mtoto wa kike kwa sababu watoto wa kike ndio waathirika wakubwa.
Kampeni hii ilikuwa na ujumbe usemao maisha yangu, haki yangu tokomeza ndoa za utotoni, kampeni hii hasa inajikita kumtetea mtoto wa kike kuepukana na unyanyasaji wa kijinsi na kupata haki zake za msingi na elimu bora.